KLABU
ya Manchester United imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji
Radamel Falcao kutoka Monaco kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Mshambuliaji huyo ataigharimu klabu hiyo Pauni Milioni 12
kwenda kuungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera
na Marcos Rojo katika orodha ya wachezaji wapya kwenye kikosi cha Louis
van Gaal.
Mchezaji
huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 tayari ameafiki
kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki na anatarajiwa kutua
Manchester wakati wowote kwa ndege binafasi kukamilisha taratibu.
0 comments:
Post a Comment