Klabu ya Manchester city jana imehitimisha safari ya vilabu vya England katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kutupwa nje na klabu ya Barcelona kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Katika mchezo wa jana Man city ilikubali kipigo cha bao moja kwa bila katika dimba la Nou camp kwa goli la kiungo Rakitic na kufanikiwa kutinga robo fainal.
Mshambuliaji wa Man city Kun Aguero alikosa penalt katika mchezo huo na hivyo kufanya matokeo ya jumla Barca kushinda kwa 3-1.
Timu zote nne za England zilizoshiriki michuano hiyo zimetupwa nje, tatu kati yao kwenye mzunguko wa pili na moja ambayo ni liverpool kwenye hatua ya makundi.
Timu zilizotolewa katika hatua ya mtoano ni Chelsea, Arsenal na Manchester city.
Sergio Aguero baada ya kukosa penalt iliyodakwa na kipa wa barca.
Wachezaji wa Manchester City wakitoka Nou camp vichwa chini.
Messi akikabwa na Martin Demichelis pamoja na wachezaji wengine wa Man City katika eneo la hatari
Haikua na jinsi mwisho wa siku ilibidi wampongeze raia huyu wa argentina Messi kwa mpira mkubwa alioupiga, wanaompongeza ni Martin Demichelis na David Silva.
0 comments:
Post a Comment