Shirikisho la soka nchini TFF leo limetoa ratiba ya
michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza tarehe 20 ya mwezi
wa tisa.
Ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji
itakayochezwa mwezi Novemba, usajili wa dirisha dogo ambao utaanza Novemba 15
hadi Desemba 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi
ya Mabingwa afrika na Kombe la Shirikisho.
Mechi za ligi msimu ujao zitachezwa wikiendi tu ili
kuongeza msisimko na kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, katikati ya
wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup), Vilevile
kutakuwa na mechi Boxing Day na siku ya Mwaka Mpya.
Ratiba hiyo inaonesha mabingwa watetezi azam fc
wataanza na wageni wa ligi Polisi Morogoro wakati Yanga wao wataanza ugenini
dhidi ya Mtibwa Suger.
Simba sc wao wataanza dhidi ya Coastal Union jijini Dare
s salaam wakati Ndanda Fc wao watafungua dhici ya Stand United mkoani Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment