Main Menu

Wednesday, August 20, 2014

RODRIGUES AFUNGUA ACCOUNT YA MAGOLI MADRID IKILAZIMISHWA SARE NA ATLETICO MADRID KATIKA SUPER CUP

REAL Madrid imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu. 


Msambuliaji Crisitiano Ronaldo hakumaliza mchezo huo baada ya kumpisha mfungaji bora wa kombe la dunia James Rodriguez ambaye aliifungia timu hiyo bao la kuongoza dakika ya 81.
James Rodriguez aliingia kuchukua nafasi ya Ronaldo na kwenda kufunga

Atletico Madrid ilikomboa bao hilo zikiwa zimesalia dakika tatu kupitia kwa Raul Garcia na sasa Real Madrid itakabiliwa na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Vicente Calderon.

0 comments:

Post a Comment