KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.
Rojo,
ambaye ametua mjini Manchester leo na kusema kuhamia United ‘anahisi
kama ndoto’, anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo
vya afya na kukubali vipengele binafsi vya mkataba wake.
Winga
Luis Nani, aliyejiunga na United kutoka Sporting kwa Pauni Milioni 17
mwaka 2007, amerejeshwa kwa mkopo klabu yake hiyo ya zamani, ikiwa ni
sehemu ya dili hilo la Rojo.
0 comments:
Post a Comment