Golikipa Mwameja Mohamed atakiongoza kikosi cha Tanzania All Stars kilichopewa jina la TSN Tanzania eleven kitakachomenyana na
magwiji wa Real Madrid ya Hispania, Agosti 23, mwaka huu.
Chini
ya makocha Charles Boniface Mkwasa na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na
viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa
kikosi hicho kitaingia kambini jumatatu ya tarehe 18 uwanja wa karume.
Wengine walioItwa ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu,
Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo,
Viungo
Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani
‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven
Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
Washambuliaji
ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid,
Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed
Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka,
Madaraka Suleiman na Akida Makunda.
Wachezaji
waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la
Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid
wanatarajia kuwasili nchini Agosti 22.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment