Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas
kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya
michezo.
afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema Kufuatia
makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya
Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia
kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini
Windhoek.
Vifaa
hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu
mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
TFF
tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa
kuendeleza mpira wa miguu nchini.
0 comments:
Post a Comment