Main Menu

Thursday, March 13, 2014

YANGA KUANDAMANA KUSHINIKIZA MANISPAA YA ILALA KUTOA MAJIBU YA MAOMBI YA ENEO LA UJENZI WA UWANJA



Klabu ya Dar es Salaam Young Africans kupitia baraza la wazee  wameipa siku tano Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwapa jibu la maombi yao ya kuongezewa eneo la Jangwani kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa michezo.

Katibu wa Baraza hilo Ibrahim Akilimali, amesema wanashangaa kuona manispaa hiyo ikiendelea kuwapiga danadana licha ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulikabidhi suala hilo kwa viongozi wa Manispaa ya Ilala.

Wazee hao wamedai katika kikao cha manispaa hiyo kilichokaa jana walishangaa kuona viongozi wao wanatolewa nje ya ukumbi wakati maombi yao yakijadiliwa ilihali walipewa mualiko.

0 comments:

Post a Comment