Wabunge wa Kenya wamesema kuwa, kuanzia leo Jumanne wataanza uchunguzi
kuhusiana na shambulio lililofanyika Septemba 21 dhidi ya kituo cha
biashara cha Westgate jijini Nairobi na kusababisha makumi ya watu
kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Asman Kamama, Mkuu wa Kamati ya
Usalama wa Taifa ya Bunge la Kenya amesema kuwa kamati za usalama wa
taifa, mahusiano ya kigeni na ulinzi zitaanza kuketi kwa pamoja na
kuchunguza tukio hilo kwa kina zoezi litakalochukua kwa akali masaa
themanini hadi kukamilika.
Kamama amewataka wananchi kujitokeza mbele ya
kamati hizo ili kutoa ushahidi walionao ambao utaweza kusaidia
uchunguzi wao kwa maslahi ya taifa la Kenya.
Amesema kuwa, uchunguzi huo
unafanyika ili kubaini kama viongozi waliopewa jukumu la kulinda
usalama wa taifa la Kenya walitekeleza majukumu yao au la.
Shambulio
hilo la kigaidi lililodumu kwa takribani siku nne lilihusisha kundi la
al Shabab la nchini Somalia.
NA radio tehran
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment