Kikosi
cha Zimbabwe kinawasili leo mchana (Novemba 18 mwaka huu) kuikabili
Taifa Stars katika mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika kesho (Novemba 19 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara
wa timu hiyo ukiwa na watu 30 utatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) saa 8 kamili mchana kwa ndege ya Kenya Airways
yenye mruko namba KQ 484 kupitia Nairobi.
Kocha
wa timu hiyo Ian Gorowa atazungumza na waandishi wa habari mara baada
ya timu hiyo kutua JNIA. Kiongozi wa msafara wa timu ya Zimbabwe ni John
Phiri.
Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni makipa; Frankson Busire, Maxwell
Nyamupangedengu na Tapiwa Kapini. Mabeki ni Carrington Nyadombo, Felix
Chindungwe, Innocent Mapuranga, Nkosana Siwela, Ocean Mushure na Patson
Jaure.
Viungo
ni Isaac Masami, Kundakwashe Mahachi, Milton Neube, Misheck Mburayi,
Obey Mwenehari na Silas Dylan Songani. Washambuliaji ni Gerald Ndlovu,
Lot Chiungwa, Nqobizitha Masuku, Simba Sithole na Themba Ndlovu.
Waamuzi
wa mechi hiyo wanatoka Uganda wakati Kamishna atakuwa Leslie Liunda wa
Dar es Salaam. Mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.
Viingilio
ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 30,000 kwa VIP
A, sh. 20,000 kwa VIP B, sh. 15,000 kwa VIP C wakati viti vya rangi ya
chungwa ni sh. 10,000.
Tiketi
zinauzwa kwenye magari maalumu katika vituo vya; Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Dar
Live Mbagala, OilCom Ubungo, Uwanja wa Uhuru, na kituo cha mafuta
Buguruni.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment