Taarifa kutoka nchini afrika ya kusini kwa aliekuwa mke wa Nelson Mandela,Winnie Madikizela zimesema kuwa Nelson
Mandela sasa ni mgonjwa sana na hawezi kuzungumza.
Winnie Madikizela ameyaambia mashirika ya habari kuwa Mandela anatumia ishara ili kuwasiliana na watu wakati Kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini akipata matibabu nyumbani kwake.
Winnie amearifu kuwa Madiba mwenye umri wa miaka 95 hajawekewa mashine za kumsaidia kuishi, Lakini hawezi kuongea kwa sababu ya mipira aliyowekewa mdomoni ili kuondoa maji maji kwenye mapafu.
Winnie ameongeza kuwa Madiba hawezi kusema chochote lakini madaktari wameahidi kuijeresha sauti yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment