Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage amesimamishwa na kamati ya utendaji
ya klabu hiyo iliyokutana jana baada ya kukiuka miiko ya uongozi na
kukiuka katiba ya klabu hiyo.
Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rage kuwasainisha mkataba
wachezaji wawili kutoka Zanzibar Ally Badru na Awadh Juma aliyekuwa
anacheza Mtibwa.
Mabosi wa Simba wamethibitisha kusimamishwa kwa Rage na wanatarajia kuliweka wazi mbele ya waandishi wa habari kwa kina.
Taarifa ya awali inadai kuwa Rage amekuwa hajishughulishi kwa karibu na
timu hiyo lakini pia amekuwa akikiiuka baadhi ya mambo ndani ya katiba
na ndio maana kamati ya utendaji imepata nguvu ya kumsimamisha kwenye
kikao hicho cha jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment