Mkutano wa nchi 20 zenye uwezo mkubwa kiuchumi
duniani, G20, unaingia siku yake ya pili na ya mwisho leo
huko St Petersburg nchini Urusi huku viongozi wa
ulimwengu wakisalia kutofautiana kuhusu mzozo wa Syria.
Rais wa Marekani, Barrack Obama, anatafuta uungwaji
mkono kutoka kwa viongozi wengine kuchukua hatua za
kijeshi dhidi ya utawala wa Syria lakini China na Urusi
zimeionya Marekani kutochukua hatua yoyote bila idhini ya
umoja wa Mataifa.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alitenga
muda jana kwenye dhifa ya chakula cha jioni kuzungumzia
mzozo wa Syria licha ya kuwa haikuwa kwenye ajenda ya
mkutano huo wa G20.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon, amesema hali ya Syria inasalia kuwa doa
katika dhamiri ya ulimwengu na kwamba mzozo wa Syria
ndio janga kubwa la kibinaadamu kwa wakati huu.
Utawala
wa Syria unashutumiwa kwa kutumia silaha za kemikali
dhidi ya raia tarehe 21 mwezi uliopita ambapo kiasi ya watu
1,400 waliuawa.
Pembezoni mwa mkutano huo wa G20,
msemaji wa rais Putin alipuuzilia mbali ripoti ya kijasusi ya
Marekani kuhusu shambulio hilo lililofanyika Damascus.
NA dwswahili
Friday, September 6, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment