Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21
mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting
Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania
Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya.
Nayo
Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini
Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi
hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu)
kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam
Complex.
Ruvu
Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa
mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati
huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi
kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi
kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda
itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati
keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar
es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi
B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso
kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi
Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22
mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi
za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi
Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora
(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui
kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu)
Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment