Main Menu

Friday, July 12, 2013

HAILE GEBRSELASSIE AJITOSA KWENYE SIASA

Mwanariadha mashuhuri wa Ethiopia Haile Gebrselassie ametangaza kujiunga na siasa kwa matumaini ya kushinda ubunge hapo mwaka wa 2015.


Tangazo hili linajiri kukiwa na duru kwamba nyota huyo wa Olimpiki anapanga kustaafu kutoka riadha. 


Haile ni mshindi mara mbili wa mbio za 10,000 katika michezo ya Olimpiki na anashabikiwa na wengi nchini Ethiopia. 


Hata hivyo hajatangaza chama cha kisiasa ambacho atatumia kuwania ubunge.


Kwa miaka mingi bunge la Ethiopia limethibitiwa na wabunge wa chama tawala cha People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF). 

Kuna mbunge mmoja pekee wa upinzani.


Akijibu mashabiki wake kupitia Twitter, Haile alisema ni kweli kwamba ananuia kujiunga na siasa mwaka wa 2015. 


Alitanagaza kustaafu mwaka wa 2010 lakini akarejea tena uwanjani na mwezi Aprili alishinda mbio za nyika za Vienna.


Pia alishiriki Marathon ya Boston iliyokumbwa na shambulio la bomu ambapo watu watatu walikufa na makumi kujeruhiwa.

chanzo bbcswahili.

0 comments:

Post a Comment