Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akiwahutuba wananchi wa Mbalizi Mbeya Vijijini jana.
CHAMA cha
demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kuanza kutoa mafunzo ya kujihami
kwa vijana wao maarufu kama Red brigedi kuanzia Agosti mosi, mwaka huu.
Akitangaza
tarehe hiyo jana wakati wa mkutano wa chama hicho uliofanyika Mbalizi wilaya ya
Mbeya Vijijini, kiongozi wa ulinzi wa chama hicho kanda ya Nyanda za juu kusini
Lucas Mwampiki, alisema kuwa ameamua kuweka wazi adhima hiyo ili serikali
isiendelee kusumbuka kuwa inao uwezo wa kuwazuia.
‘’Polisi
msisumbuke kutafuta kuwa tutaanza lini, ni hivi, tutaanza tarehe 1, mwezi wa
nane mwaka huu’’ alisema Mwampiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwakibete
Jijini Mbeya.
Mgeni rasmi
katika mkutano huo Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na
Mbunge wa Arusha mjini, alisema amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa vijana
waliohitimu mafunzo ya JKT na kuachwa bila ajira ili wajiunge na mafunzo hayo.
‘’Nimekuwa
nikipokea simu nyingi za vijana waliohitimu JKT na kuachwa mitaani wakiomba
kujiunga na mafunzo ya Redbrigedi huku wakiuliza kiingilio’’ alisema Lema.
Alisema kuwa
ijulikane kuwa mtu anapozuia demokrasia anazalisha waasi na Chadema hawapo
tayari kuuawa kijinga.
Mbali na
suala hilo, Lema alisema alishangazwa na uandishi wa vyombo vya habari hapa
nchini katika ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama, ambapo Magazeti mengi
yaliandika habari za kushikana viuno na mkewe badala ya kuandika jambo ambalo
alijia.
‘’Waandishi
wa Tanzania badala ya kuandika alichojia Obama, wao waliishia kupiga picha
akiwa ameshikana na mkewe na kuweka front page huku madini yakiondoka na Rais
Kikwete akiongoza kuomba Kondomu na kusaini mikataba ya kutorosha madini yetu’’alisema
Lema huku akishangiliwa na wananchi zaidi ya 2000 waliohudhuria mkutano huo
wakiwemo viongozi wa CCM.
Aliwaambia wanachama
wa Chadema kuwa waache kuwachukia wanachama wa CCM bali wawaelimishe taratibu
maana hata ukitaka kupata kifaranga huwezi kununua yai dukani na kulipasua
kisha ukapata kifaranga bali mpaka yai hilo liatamiwe na kuangaliwe.
Mbunge wa
Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, alisema kwa sasa anakubali kuwa yeye ni ‘’Rais wa
Mbeya’’ kutokana na wananchi kumkubali na kwamba CCM wasitarajie kulikomboa
Jimbo la Mbeya Mjini mwaka 2015 na aliwashukuru sana Polisi wa Mbeya kwa kuacha
kuisaidia CCM.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo wa kuimarisha chama katika kata ya
Nsalala na Utengule Usongwe Kissman Mwangomale (KK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kijiji cha Mshikamano kata ya Nsalala, alisema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda
anapaswa kujiuzulu kwasababu alitamka kuwa amechoka.
‘’Pinda
anapaswa ajiuzulu maana alitamka kuwa amechoka, sisi hatujachoka tuna uwezo wa
kuongoza dola aachie ngazi au afute haraka kauli yake’’ alisema Mwangomale.
Naye diwani
wa kata ya Iyela ya Jijini Mbeya Charles Mkela, aliwashukuru wanachama wa CCM
kumpigia kura nyingi za ndiyo katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni
na kukiwezesha Chadema kushinda.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwemo Frank Mwaisumbe ambaye
ni Mratibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini na viongozi kutoka Mbeya
mjini na wilaya ya Mbozi.
Lema akiwa na baadhi ya viongozi wa Chadema Mbeya. Hapa ni jana mjini Mbalizi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mshikamano mjini Mbalizi kata ya Nsalala Mbeya
Vijiini Kissma Mwangomale (KK) akihutubia mkutano kwenye viwanja vya
mahubiri.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwahutubia wananchi wa Mbalizi jana.
Mratibu wa M4C Frank Mwaisumbe akiwahutubia wananchi wa Mbalizi Mbeya vijijini jana.
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya mjini John Mwambigija, akiwahutubia wananchi Mbalizi.
Lema akiwa na baadhi ya vijana wa Redbriged Mbalizi Mbeya jana.
Lema akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chadema wilaya ya Mbeya vijijini mkoani Mbeya baada ya kushuka kwenye ndege.
Lema akipokelewa na wanachadema uwanja wa ndege Songwe mkoani Mbeya jana.
Lema kulia akifuatiwa na Sugu kisha viongozi wengine mkoni Mbeya jana
Godbless Lema akiwa ameshuka uwanja wa ndege Songwe Mbeya jana
taarifa hii kwa hisani ya kalulunga.blogspot
0 comments:
Post a Comment