Main Menu

Sunday, May 5, 2013

TP MAZEMBE YATUPWA NJE YA MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA

Klabu ya TP Mazembe, ya Jamuhuri Yakidemocrasi ya Congo, imebaundiliwa nje ya michuano ya kluwania kombe la klabu bingwa barani Afrika na Orlando Pirates ya Afrika Kusini licha uya kuilaza bao moja kwa bila katika mechi iliyochezwa mjini Lubumbashi.

Licha ya Ushindi huo, TP Mazembe, inayaaga mashindano hayo, kwa kuwa Orlando Pirates, ilishinda mechi ya raundi ya kwanza kwa mabao mabao matatu kwa moja.

Orlando Pirates sasa imefuzu kwa raundi ya mchujo na jumla ya magoli matatu kwa mawili.

Shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF linatarajiwa kutoa droo ya ruandi hiyo ya mchuzo wiki ijayo.

Nchini Burundi, Kilabu ya Lydia Liduc Academi, imefuzu kwa raundi ya mchujo wa kuwania kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuishinda timu kongwe ya Asec Mimosa d' Abidjan ya Cote d Ivoire katika raundi ya pili ya fainali za kombe hilo.

Lydia Lidic imekuwa ni timu ya kwanza kutoka Burundi kufikia hatua hiyo kwa zaidi ya miaka 22. 

Na ni timu pekee ya Afrika ya Mashariki na Kati iliosalia kwenye mashindano hayo.

0 comments:

Post a Comment