Imekua sasa ni Jambo la kawaida kabisa kwa Wabunge wa CCM kujibu hoja za
Wabunge wa Upinzani hususan CHADEMA, badala ya Serikali kujibu.
Tulishuhudia juzi katika Hotuba ya Wizara ya Mali Asili na Utalii
iliyowasilishwa na Waziri Kivuli wa Wizara hiyo Mch Peter Msigwa.
Katika
hotuba hiyo iliyokua ikielezea jinsi Katibu Mkuu wa CCM Abdrahaman
Kinana anavyohusishwa na Ujangili wa Tembo hakuna hata Mbunge mmoja wa
CCM aliechangia kwa kuomba au Kuiyagiza Serikali Kuchunguza yale
yaliyosemwa na Mch Peter Msigwa kama yana Ukweli ili Serikali imchukulie
hatua Katibu huyo wa CCM!
Wemgi wa wabunge hawa wa CCM waliishia Kurusha Vijembe kwa Msigwa na
Kumtetea Kinana na Serikali. Tulimuona Emmanuel Nchimbi waziri wa mambo
ya ndani akiwa wa kwanza kumtetea Kinana, badala yeye akiwa kama Waziri
mwenye Dhamana na Mambo ya ndani ya Nchi kumuomba Mh Peter Msigwa huo
Ushahidi dhidi ya Kinana kuhusika na Ujangili wa Tembo.
Alifikia hata
hatua ya Kumkashifu Msigwa na sio yeye tu hata Wabunge wengine wa CCM
walichofanya ni Kujibu hoja za serikali na Kumtetea Kinana.
Kazi ya Bunge ni kuishauri kuiamuru na Kuisimamia Serikali katika mambo
yote yanayohusu maswala ya Nchi na Wananchi kwa ujumla. Ila kwa Bunge la
sasa imekua tofauti kwani wanachofanya Wabunge haswa wa CCM ni
KUITETEA serikali na kuchukua nafasi ya Serikali Kujibu Hoja za Wabunge
hususan wa CHADEMA.!
Ndio maana Serikali imekua haiwajibiki kwa Wananchi ipasavyo kutokana na
kundi hili la wabunge wa CCM kuisaidia kujibu hoja za Wapinzani. Kuna
haja katika Katiba ijayo Waziri asiwe Mbunge ili hili tatizo la Wabunge
wa chama kinachounda Serikali wasiwe wanawatetea Mawaziri kwa kua tu
wanatokana na chama chao..!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment