Zoezi la kuhesabu kura katika uchaguzi wa rais
nchini Kenya linaendelea, huku matokeo ya awali
yakionyesha Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta
akiwa mbele ya mpinzani wake, Waziri mkuu Raila
Odinga.
Ikiwa karibu theluthi moja ya kura
zimekwisha hesabiwa, Kenyatta alikuwa na asilimia
54 na Odinga asilimia 41, huku wagombea wengine
wakiwa mbali mno.
Hata hivyo, wachambuzi
wametahadharisha kuwa maeneo mengi ambayo
yamewasilisha matokeo ni yale yanayomuunga
mkono Kenyatta.
Mbali na kumchagua Rais, wapiga
kura pia wamewachagua wabunge, maseneta,
magavana na madiwani. Matokeo ya awali
yameshatoa washindi katika baadhi ya wilaya,
ambapo wagombea kadhaa wamekubali kushindwa.
Wapiga kura milioni 14.3 walijiandikisha, na mwitikio
ulitarajiwa kuvuka asilimia 70 iliyofikiwa mwaka 2007.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment