Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars)
iliyopo kambini kisiwani Zanzibar, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na
timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23, 2015.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika uwanja wa Aman
Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na
fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini
Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.
Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili katika
viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kujiandaa
na fainali hizo za michezo ya afrika, wachezaji wote waliopo kambini wapo
katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment