Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles
Mkwasa watakua wakijifua mara mbili kwa siku asubuhi na jioni katika uwanja wa
Karume katika kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.
Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao
kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa
amewaongeza wachezji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.
Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kocha mkuu
pamoja na benchi lake la ufundi kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika
mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa
kambi ya siku kumi.
Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi leo ni Said
Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba
SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu
(JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan
Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu
Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).
0 comments:
Post a Comment