Mabingwa mara tano wa michuano ya Kombe la Kagame timu ya
Young Africans leo imefufua matumaini ya kutinga robo fainal ya michuano hiyo
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka
nchini Djibout, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu
aliyefunga mabao mawili, na Geofrey Mwashiuya aliyefunga bao la tatu kwa
kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.
Katika
mchezo wa leo Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake
Amissi Tambwe na Saimon Msuva katika kipindi cha kwanza.
Katika
mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa
mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka
na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment