Friday, July 3, 2015
SIMBA AAJIRI KOCHA WA MAZOEZI YA VIUNGO KUTOKA SERBIA
Klabu ya Simba leo imeingia mkataba na kocha mpya wa mazoezi ya viungo Dušan Momčilović.
Kocha huyo kutoka Nchini Serbia ana uzoefu mkubwa katika fani ya mpira wa miguu hususani mazoezi ya viungo.
Kocha Dušan amefundisha klabu mbalimbali duniani kwenye Nchi kama Malaysia, Indonesia, Georgia ambako Alikuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa klabu ya FC DINAMO ambayo ilicheza mechi za awali ya klabu bingwa ya Ulaya-UEFA, Bosnia and Herzegovina, Oman na Belgrade
Kocha Dušan pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
Kocha Dušan ni muhitimu wa Digrii ya Mazoezi ya Viungo jijini Belgrade akiwa amejikita Zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kujenga mwili.
Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha Dušan Momčilović mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment