Michuano ya Copa Amerika itafikia tamati leo kwa mchezo
wa fainali kati ya wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Chile na timu ya
taifa ya Argentina.Hakika hili ni bonge la fainali.
Hii itakuwa fainali ya tano kwa timu ya taifa ya Chile
katika michuano ya kombe la Amerika ya kusini kwani tayari Chile
wamekwishacheza fainali nne za michuano hiyo.
Timu ya taifa ya Chile ina rekodi ya kucheza fainali nne
za michuano ya Amerika Kusini pasipokutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Fainali walizocheza
Chile katika michuano ya Copa Amerika ni mwaka 1955 walipofungwa na timu
ya taifa ya Argentina goli moja kwa sifuri goli lililofungwa na na Rodolfo
Micheli dakika ya 59.
Fainali nyingine walizocheza Chile ni za mwaka 1956
wakifungwa na Uruguay,mwaka 1979 wakifungwa na timu ya taifa ya Paraguay na mwaka 1987 wakifungwa na timu ya taifa ya
Uruguay goli moja kwa sifuri goli la Pablo Bengoechea katika dakika ya 56.
Endapo Chile watachukua ubingwa wa Copa Amerika mwaka huu,utakuwa
ubingwa wao wa kwanza wa michuano hiyo.
Vipi kwa wapinzani wao timu ya taifa ya Argentina?Kwa
Argentina hii ni fainali yao ya 27 ya
michuano ya Copa Amerika huku wakichukua mara 14 na mara 12 wakiwa washindi wa
pili.
Mara ya mwisho kwa Argentina kuchukua ubingwa wa michuano
ya Copa ni mwaka 1993 wakiwafunga Mexico
Magoli 2-1.
Magoli ya Argentina katika mchezo huo, magoli ya
Argentina yalifungwa na Gabrile ‘Batigol’
Batistuta magoli mawili huku goli la kufutia machozi kwa upande wa
Mexico likifungwa na Benjanmin Galindo.
Endapo Argentina watachukua ubingwa wa michuano ya Copa
Amerika mwaka huu watafikia rekodi ya Uruguay ya kuchukua ubingwa wa michuano
hii mara 15.
Timu za Argentina na Chile zimekutana mara 85 katika
mashindano yote na Argentina imeshinda mara 57, mara 22 zikienda sare na Chile
ikishinda mara 8 tu.
Mara ya mwisho timu hizi zimekutana katia hatua ya kufuzu
katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2012 nchini Brazil.
Katika mchezo huo,Argentina walishinda magoli 2-1 kwa
magoli ya Lionel Messi na Gonzalo Higuain.
Zipo takwimu nyingi zinazohusu timu hizi za Chile na
Argentina katika mashindano haya ya Copa Amerika mwaka huu.
Chile ndiyo timu iliyofunga magoli mengi katika michuano
hii ya Copa Amerika zaidi ya Argentina.Chile imefunga magoli 13 mpaka sasa huku
Argentina wakifunga magoli 10 pekee.
Wakati Chile wakiongoza kwa kufunga magoli mengi katika
michuano ya Copa Amerika,timu hiyo pia ndiyo iliyoruhusu magoli mengi ya kufungwa kuliko timu ya taifa ya
Argentina.
Chile wamefungwa magoli 4 katika michuano hiyo tofauti na
magoli 3 waliyofungwa Argentina katika michuano hiyo.
Timu zote mbili zimefungana katika kucheza michezo 3
pasipo kuruhusu goli kwa makipa Claudio Bravo wa Chile na Sergio Romeo wa
Argentina.
Lionel Messi ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupiga
mashuti mengi golini akiwa amepiga mashuti 17 akifuatiwa na EDUARDO Vargas na
Arturo Vidal Pado wa Chile wenye mashuti
14 yaliyolenga goli kila mmoja.
Messi pia anashikilia rekodi ya kupiga pasi nyingi za magoli pamoja na kiungo wa
chile Jorge Valvidia wakipiga pasi 3 kila mmoja.
Hii itakuwa ni fainali ya pili kwa Argentina na Chile
kukutana kwani tayari walikwishakutana mwaka 1955 na Argentina kushinda mchezo
huo.Je,tutegemee Chile kulipa kisasi kwa Argentina?
0 comments:
Post a Comment