Kikosi cha timu ya
Taifa ya vijana umri chini ya miaka 15 (U-15) kitaingia kambini siku ya
jumatatu tarehe 22/06/2015 ili kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya
kombaini ya mkoa wa Mbeya, mchezo utakaofanyika mjini Mbeya jumatatu ya tarehe
28/06/2015.
Kikosi hiki
kinaandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na na michuano ya mtoano kuwania kufuzu kwa
fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyia nchini
Madagascar mwaka 2017. Hatua ya mtoano wa awali itaanza mwakani 2016 mwezi
Juni.
Timu itakua chini ya
kocha Bakari Shime kwa muda akisaidiwa na Peter Manyika. Kocha aliyekua
ameteuliwa awali kufundisha timu hiyo Adolf Rishard ameomba udhuru baada ya
kupata fursa ya kwenda masomoni.
Wachezaji
watakaoingia kambini na mikoa wanayotokea kwenye mabano ni Mwijuma Yahya
(Tanga), David Mpakazi, Shilole Anthony (Geita), Kibwana Shomari ,
Ibrahim Koba, (Morogoro), Faraji John, Kelvin Deogratius, Davison Meddy ,
Maulid Lembe (Dodoma), Ally Msengi (Mwanza).
Wengine ni Timoth
Timothy, Juma Juma, Pius Raphael, Mohamed Ally (Dodoma), Athumani Rajabu, Juma
Zubeir, Jonathan Rafael (Kigoma), Robert Philip, Jaffari Juma (Arusha), Michael
Kanuti, Alex Peter, Rashid Kilongola (Kinondoni), Morris Michael (Ilala), Karim
Mfaume (Lindi), Assad Juma (Unguja Magharibi), Francis Mrope, Kelvin Pius
(Mara)
0 comments:
Post a Comment