Main Menu

Thursday, June 18, 2015

CAF YAMUONDOA NGASSA TIMU YA TAIFA



Mrisho ngasa akiwasili visiwani zanzibar na wachezaji wenzake wa stars mapema leo


Winga mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichoenda Zanzibar kupambana na Uganda siku ya jumamosi.

Shirikisho la Mpirani wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa mwongozo kuwa mchezaji Mrisho Halfan Ngasa haruhusiwi kucheza CHAN kwa sababu sio mchezaji tena wa ndani.

Mapema baada ya kumalizika kwa ligi kuu Tanzania bara ngassa alisajiliwa na timu ya Free State ya nchini afrika kusini na hivyo hatambuliki tena kama mchezaji wa ndani.

Awali ngassa alikua akiichezea timu ya young Africans, Hata hivyo ngasa yupo visiwani zanzaibar.

0 comments:

Post a Comment