Timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku
ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.
Msafara wa Taifa
Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika
hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani
kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.
Stars inakutana na
Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa
Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda,
kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Mara baada ya kurejea
kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya
Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo
asubuhi kuelekea visiwaniZanzibar.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij
amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya
Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo
huo wa CHAN wikiendi hii.
Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green,
Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na
wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum
Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.
Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi
Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John
Bocco.
Waaamuzi wa mchezo
huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda),
akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi
wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye
kutoka Kenya.
0 comments:
Post a Comment