Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi
na jioni katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo
dhidi ya Misri.
Jana kikosi cha Stars
kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia
(Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.
Taifa Stars ambayo
imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa
kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu
ya taifa ya Misri.
Daktari wa Taifa
Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi
ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika ukanda wa juu
(mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa
ajili ya mchezo.
Hali ya hewa ya
Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari
ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis
Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.
Wachezaji wote wa
Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra
na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.
Wenyeji Chama cha
Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo
mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misri.
0 comments:
Post a Comment