Kikosi cha Taifa Stars kimeendelea
na mazoezi katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo
utakaopigwa kuanzia majira a saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Stars inahitaji ushindi katika
mchezo huo wa awali ili kujiweka katika mzingira mazuri ya kusonga mbele, kabla
ya mchezo wa marudaino utakaofanyika baada ya wiki mbili jijini Kampala.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart
Nooij amesema vijana wake wako katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho,
na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti katika mchezo huo.
Endapo Stars itaitoa Uganda katika
hatua ya awali, itafuzu katika hatua ya pili ambapo itacheza dhidi ya timu ya
Taifa ya Sudan, na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu kwa fainali za
CHAN 2016 nchini Rwanda.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya
Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili leo mchana jijini Dar es salaam kisha
kuelekea kisiwani Zanzibar tayari kwa mchezo huo wa kesho dhidi ya Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment