Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya
kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya
Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar,
Baadhi ya maamuzi yake ni haya
yafuatayo:
1.
TUNZO ZA
VODACOM.
Baada ya kuzingatia mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi
wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza
Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za
Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF
katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi
hili.
1.
KANUNI ZA LIGI
2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu,
FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:
1.
LESENI ZA VILABU.
Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu
itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club
Licencing).
1.
WAAMUZI.
Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa
kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees)
litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.
Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa
akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).
1.
MGAWANYO WA
MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato ya milangoni na
sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni
18% VAT na 15% gharama za uwanja.
1.
UDHIBITI WA
WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji
asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.
1.
KUSAJILI
MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu
itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa
muhuri na lakiri ya TFF na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na
mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya kusajiliwa na TFF.
1.
WACHEZAJI WA
KIGENI.
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi
ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba)
wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.
Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
a.
Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za
Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
b.
Mchezaji awe anacheza katika ligi
kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
1.
Kila mchezaji wa kigeni
atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa
kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa
maendeleo ya mpira (Football Development Fund).
Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai
itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini
wataruhusiwa kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na
vilabu vyao.
4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua kuwa
kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au
itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha
msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu.
Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa
Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka
katika mashirikisho mengine duniani.
Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF
imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa maendeleo ya
mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.
0 comments:
Post a Comment