Fainali ya kwanza ya Ligi ya mpira wa kikapu ya NBA
nchini Marekani imetimua vumbi hii leo kwa mchezo kati ya Cleveland Cavaliers
na Golden State Warriors.
Katika mchezo huo,Golden State Warriors wameshinda katika
muda wa nyongeza kwa pointi 108 dhidi ya 100 za Cleveland Cavaliers.
Pamoja na nyota wa Cleveland Lebron James kufunga pointi
44, bado hazikuweza kuwasaidia Cleveland kushinda mchezo wao huo dhidi ya
Golden State Warriors.
Mchezo wa pili wa fainali utachezwa siku ya jumapili ya tarehe
saba mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment