MSHAMBULIAJI
wa timu ya Stand
United,Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari mkoani
Tanga mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya
Coastal Union,Picha na Mwandishi Wetu,Tanga
Mshambuliaji wa timu ya Stand United,Abasarim
Chidiebele amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa
mwaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Chidiebele alitua mkoani
Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union
ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa
Coastal Union,Kassim El Siagi,Meneja wa Coastal Union,Akida Machai na viongozi
wengine.
Akizungumza mara baada ya
kusaini,Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na
kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo
katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.
“Nashukuru kusajili
Coastal Union kikubwa niwahaidi tu wapenzi,wanachama na mashabiki kutumia uwezo
wangu katika kuipa mafanikio timu yetu “Alisema Mshambuliaji huyo ambaye ni
tishio hapa nchini.
Kwa upande wake,Ofisa Habari
wa Klabu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa msimu huu timu hiyo
imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha kuhakikisha wanachukua
ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
“Unajua usajili
wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio itakuwa njia
pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu
msimu ujao “Alisema.
Hata hivyo aliwataka wapenzi
mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo
yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika
michuano ya Ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment