Kocha wa viungo wa Azam Fc Mario Marineka (kushoto) Jaffar Idd Maganga na didier Kavumbagu (kulia) baada ya mazoezi.
Mshambuliaji wa timu ya Azam Fc mrundi Didier Kavumbagu ametoa
sababu za kushindwa kufanya vizuri katika msimu wa pili wa ligi kuu
uliomalizika mwezi uliopita.
Akizungumza
na mtandao huu kavumbagu amesema mabadiliko ya mwalimu ndio sababu kubwa na yeye
kushindwa kufanya vyema mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom.
Ikumbukwe
wakati ligi inaelekea mzunguko wa pili Kavumbagu alikua na magoli kumi lakini
alijikuta akishindwa kupasia nyavu tena na kumpa nafasi Simon Msuva na Amisi Tambwe
kumpita.
Didier
amesema sababu nyingine ni ya kifamilia ambayo ilimfanya wakati mwingine akili
yake kutokua vyema na kushindwa kupaform.
Katikati
mwa msimu uliopita Azam Fc walimtimua kocha wake Mcameroon Joseph Omog baada ya
timu hiyo kushindwa kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa ya klabu bingwa
afrika baada ya kutolewa na El Merrekh ya Sudan.
Kavumagu
ndie mchezaji pekee wa kigeni aliyejiunga na kikosi cha Azam kilichoanza
mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kagame.
0 comments:
Post a Comment