Main Menu

Saturday, May 30, 2015

COASTAL UNION YAWAPIGA CHINI WACHEZAJI WAKE ZAIDI YA KUMI


 
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Coastal Union ambacho kimeketi katikati ya wiki hii chini ya Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto kimeazimia kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao muda wao ulikuwa umemalizika huku wengine wakiongezewa mikataba ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.

Kimsingi wachezaji hao wameachwa na sasa wapo huru kutumikia timu nyengine ambazo zitahitaji huduma zao

Ofisa Habari wa Coastal Union, Oscar Assenga amesema kuwa maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ambacho kilifanyika juzi mkoani humo.

Amesema kuwa kimsingi katika kikao hicho kiliridhia kuwaacha wachezaji waliomaliza mikataba yao ikiwemo Shabani Kado,Keneth Masumbuko,Yayo Kato Lutimba, Seleimani Kibuta,Bakari,Razack Khalfani,Itubu Imbem na
Othumani Tamimu.

Aidha amesema kuwa wachezaji wengine ambao klabu imeamua kuwaacha ni Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamedi Mtindi na Mohamed Hassani.

Hata hivyo amesema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ambao klabu ipo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya msimu ujao ni Bakari Mtama,Rama Salim, Godfrey Wambura na Joseph Mahundi.

Wakati huo huo, uongozi wa Coastal Union  umewapandisha timu wachezaji wanne kutoka timu ya vijana kucheza timu ya wakubwa ambao ni Mtenje
Albano, Tumaini Karim, Mohamed Twaha Shekue “Djong”, Fikirini Suleiman“Mapara”

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.

0 comments:

Post a Comment