Hatimae
Joseph Sepp Blatter amefanikiwa kutetea kiti chake cha urais wa shirikisho la Soka
Duniani FIFA baada ya kumuangusha mpinzani wake mwana wa Mfalme Ali Bin Al Husein.
Katika uchaguzi
huo uliofanyika katika jiji la Zurich Uswiss blatter amepata kura 133 dhidi ya
73 za mpinzani wake katika Round ya kwanza.
Kutokana na
matokeo hayo upigaji kura ulitakiwa urudiwe lakini Prince Ali akajitoa na kumpa
nafasi Blatter kutangazwa mshindi.
Kwa matokeo
hayo Blatter mwenye umri wa miaka 79 ataongoza kwa miaka 4 akikabiliwa na
changamoto ya tuhuma za rushwa zinazowakabili maofisa wa taasisi hiyo,
uchunguzi unaoendeshwa na mamlaka za marekani.
Lakini pia
atakabiliwa na tishio la UEFA la kugomea michezo ya kufuzu kwa kombe la dunia
la mwaka 2018, tishio lililotolewa na rais wa UEFA Michel Platini siku ya
alhamisi.
Naye mwenyekiti
wa fa ya England Greg Dyke aliiambia Sky News kuwa England itajiondoa katika
michuano ya FIFA kama Blatter ataendelea kuongoza.
Kwa madai
kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kutokea chini ya Blatter ambaye
ameshakaa madarakani kwa miaka 16.
Katika hotuba
yake baada ya ushindi Blatter amemshukuru na kumpongeza mpinzani wake kwa
kusema alikua mshindano wa kweli.
Kuhusu sakata
la rushwa linaloshikiliwa kidete na Marekani na Uingezeza, Blatter amesema kama
mataifa hayo yangepata nafasi ya kuandaa kombe la dunia hayo yote yasingetokea.
0 comments:
Post a Comment