Wakati timu mbalimbali zikiboresha
vikosi vyao, uongozi wa timu ya stand united bado unasubiri ripoti ya kocha ili
ili kuzingatia mapendekezo yake.
katibu msaidizi wa klabu hiyo Kenedy
Nyange amesema pamoja na kusubiri ripoti ya mwalimu bado hali ya kifedha sio
nzuri japo wapo kwenye mazungumzo na wadhamini wanaotaka kuwekeza kwenye timu
hiyo.
Amesema hawashangai timu nyingine
zikiwa zimeanza usajili kwa sababu yawezekana ripoti za makocha wao
zinawaruhusu lakini akashangazwa pia na timu ambazo hazina kocha na zinafanya
usajili.
Stand United inayofundishwa na kocha
raia wa Uganda Mathius Lule, ilisalia ligi kuu msimu huu baada ya kupata
ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting.
0 comments:
Post a Comment