Kocha
Jackson Mayanja wa Kagera Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa
mechi tatu kwa kutoa lugha ya kashfa kwa maneno na vitendo kwa waamuzi wa mechi
yao na Mtibwa Sugar kuwa walipewa rushwa.
Adhabu
dhidi ya Kocha Mayanja kwenye mechi hiyo namba 136 iliyochezwa Aprili 1, 2015
kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya
40(1) ya Ligi Kuu.
Klabu
ya Mtibwa Sugar imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya timu yake kukataa
kuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi namba 142 dhidi ya Stand
United iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14(13) ya Ligi
Kuu.
Nayo
Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu
baada ya timu yao kugoma kuingia kwenye vyumba vya kuvalia nguo (changing room)
kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa mechi dhidi ya Kagera
Sugar.
Hatua hiyo ilisababisha wachezaji wakaguliwe kwenye gari lao.
Pia
Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kuzingatia kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu
baada ya vilevile kugoma kuingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo
hiyo namba 146 iliyochezwa Aprili 6, 2015.
Kipa
Tony Kavishe wa Polisi Morogoro amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa
mechi tatu kwa kosa la kumpiga ngumi mwamuzi msaidizi namba mbili, Hassan Zani
kwa kuzingatia kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu. Alifanya kosa hilo kwenye mechi
namba 147 dhidi ya Mgambo Shooting iliyochezwa Aprili 5, 2015 katika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment