Kocha Emanuel Masawe (katikati) akizungumza na wachezaji wake katika chumba cha kubadilishia nguo.
Kocha wa
timu ya Stand United aliyesimamishwa na uongozi wa timu hiyo Emanuel Masawe amesema
milango ipo wazi kwa timu yoyote inayohitaji huduma yake.
Masawe ambaye
hivi karibuni aliripotiwa kutua kuifundisha timu ya Polisi Moro amesema tangu
uongozi wa Stand United ulipotangaza kumsimamisha haujampa barua yoyote ya
kusimama kwake.
Amesema yeye
bado ni kocha wa timu hiyo ambayo aliipandisha ligi kuu kutoka ligi daraja la
tatu hadi pale mkataba wake utakapo malizika mwezi wa saba.
Katika kusisitiza
hilo amesema hata alivyokwenda kufanya mazungumzo na uongozi wa timu ya Polisi
Moro aliwataarifu viongozi wa Stand ambao kimsingi bado ana mkataba nao.
Hata hivyo Masawe
amesema mazungumzo yake na uongozi wa Polisi Moro hayakufikia muafaka na hivyo
kushindwa kufanya nao kazi huku akiahidiwa kuitwa msimu ujao kama itafanikiwa
kubaki ligi kuu.
Masawe ambaye
ana leseni Class B ya caf anasema hivi sasa yupo tayari kufanya kazi na klabu yoyote sehemu yoyote barani Afrika ambapo
leseni yake inamruhusu.
Emanuel Masawe
ambaye anamkubali zaidi kocha Sunday kayuni wa Tanzania na Jose Mourihno wa Chelsea
japo hapendi style ya uchezaji wake ni kaka wa mchezaji wa Ndanda Fc Jacob Masawe.
0 comments:
Post a Comment