Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
TFF iliyokutana Aprili 19, 2015 imepanga kusikilizwa kwa rufaa ya Damas
Ndumbaro Mei 10 mwaka huu, makubaliano ambayo yalifikiwa na pande zote mbili
kwa pamoja.
Kikao hicho kilipitisha taratibu za kisheria ambazo
zitatumika kuamua kesi hiyo, ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani
ikiwemo kuwasilisha hoja kwa mdomo na si maandishi, kitendo ambacho
kimekubaliwa na pande zote mbili.
Utaratibu huu umekua ukitumika katika mahakama za kawaida
kuepusha manung'uniko kwa upande mmoja kulalamika umeonewa.
0 comments:
Post a Comment