Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam
DRFA, kimetangaza zawadi kwa washindi wa michuano ya ligi ya wanawake mkoa wa
Dar es salaam inayoendelea katika viwanja mbalimbali Jijini.
Mwenyekiti wa chama hicho Almas
Kasongo,amesema zawadi hizo zitatolewa kwa mshindi wa kwanza na wapili,mchezaji
bora wa mashindano,mfungaji bora,kipa bora,timu yenye nidhamu na mwamuzi bora.
Mshindi wa kwanza atazawadiwa
Kikombe,jezi seti moja na kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano
(1,500,000/=), Mshindi wa pili atapata jezi seti moja na kiasi cha shilingi
laki saba (700,000/=) ,Mchezaji bora wa mashindano atazawadiwa kiasi cha
shilingi laki mbili (200,000/=), Mfungaji bora atapata shilingi laki moja na
nusu (150,000/=),Kipa bora atapata shilingi laki moja na nusu (150,000/=),Timu
yenye nidhamu itazawadiwa shilingi laki nne (400,000/=),huku mwamuzi bora
akiondoka na shilingi laki mbili (200,000/=).
Ligi hiyo yenye jumla ya timu 8
imeanza kutimua vumbi jumapili ya April 19/2015,kwa mchezo wa ufunguzi
uliozikuwanisha timu za Temeke Squad dhidi ya Ever-Green Queens,na kushuhudiwa
Ever-Green ikichomoza na ushindi wa kishindo wa mabao 5-1,yaliyofungwa na Sherida
Boniface dakika ya 7,19na 39,na mengine yakifungwa na Donicia Daniel katika
dakika ya 60 na 65,na lile la kufutia machozi kwa Temeke Squad likifungwa na
Aisha Juma.
Tumi zote zinzoshiriki michuano hiyo
ya ligi ya wanawako mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na
IMETOLEWA NA DRFA,
Omary Katanga Mkuu Wa Habari Na
Mawasiliano,DRFA
0 comments:
Post a Comment