Timu za Bayern Munich ya Ujerumani na Barcelona ya Uhispania
zimefanikiwa kusonga mbele kwa kutinga nusu fainali mashindano ya Klabu
Bingwa Barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao hapo jana usiku.
Baada
ya kuchezea kichapo cha cha bao 3-1 katika mechi ya awali dhidi ya FC
Porto ya Ureno ugenini, hatimaye Bayern Munic waliigeuzia kibao Porto
na kuirarua bila huruma mabao 6-1 na hivyo kuwa na njia nyeupe ya
kutinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 7-4.
Nao Barcelona
baada ya ushindi wa awali wa bao 3-1 dhidi ya PSG mjini Paris, hapo jana
imeendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza kwa
mabao bao 2-0, yaliyotiwa wavuni na Mbrazil Neymar katika kipindi cha
kwanza.
Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa
jumla ya magoli 5-1.
Mechi nyingine za robo fainali zinakamilika hii
leo, pale Juventus ya Italia itakaposhuka uwanjani kumenyana na AS
Monaco ya Ufaransa, huku shughuli nyingine pevu ikitarajiwa kuonekana
kwenye dimba la Santiago Bernabeu, pale mabingwa watetezi Real Madrid
watakapo wakaribisha watani wao wa jadi Atletico Madrid.
Katika mechi ya
awali mafahali hao wawili walitoka suluhu ya bila kufungana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment