Klabu ya soka ya Yanga imetangaza viingilio vya mchezo
wake dhidi ya Etoile du Sahel utakaofanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa
taifa Dar es salaam.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Jerry
Murro amesema kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakua shilingi 5,000.
Kiingilio cha juu ni shilingi 40,000 ambapo itakua VIP A,
VIP B shilingi 30,000, VIP C shilingi 20,000 na jukwaa rangi ya chungwa
shilingi 10,000.
Murro amesema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho
katika vituo mbalimbali jijini Dar es
salaam.
Baadhi ya vituo hivyo ni uwanja wa Karume, Ubungo stand, Dar
live Mbagala, Mwembe Yanga, Buguruni sheli, Feri kivukoni, Bilicanas na makao
makuu ya klabu ya Yanga.
0 comments:
Post a Comment