Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mholanzi Hans Van Pluijm amesema
mchezo wake dhidi ya timu ya Etoile du Sahel ni kama vita.
Hans amesema kwa upande wao maandalizi yapo vizuri hakuna
wachezaji wenye majeruhi makubwa zaidi ya Salum Telela ambaye anaendelea vizuri.
Amesema anaamini vijana wake watafanya vizuri japo
anawaheshimu etoile kwa kuwa ni timu yenye uzoefu mkubwa na michuano ya Afrika.
Kuhusu muda wa kuchezwa mchezo huo Hans amesema utachezwa
saa kumi kamili muda ambao wamezoea kucheza na sio saa tisa kama ambavyo
iliripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Timu ya Etoile inatarajiwa kuwasili kesho saa tisa usiku
kwa ndege ya kukodi wakiwa na msafara wa watu 55.
Yenyewe Yanga imeweka kambi katika hotel ya Tasoma iliyopo
jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment