Shujaa wa zamani wa timu ya Manchester United Eric Cantona
amefurahishwa na ushindi walioupata Man U wikiendi iliyopita katika ile Manchester
Derby na sasa anaamini timu hiyo msimu ujao wa 2015/2016 itatwaa ubingwa wa
EPL.
Legendary
huyo aliyeichezea Man U miaka ya tisini anaamin timu yake itashinda taji la
ligi msimu ujao.
Louis van Gaal na vijana wake wanashika nafasi ya tatu wakiwa pointi nane nyuma ya viongozi Chelsea, kufuatia ushindi wa michezo sita mfululizo waliupata na kuwaweka umbali wa point nne juu wa timu inayoshika nafasi ya nne na alama nane kwa timu inayoshika nafasi ya tano.

Cantona ametoa kauli hiyo alipokua akizungumza katika tuzo za Laureus World Sports jijini Shanghai mapema leo.
Mfaransa huyo ambaye alishinda makombe manne ya ligi kuu na mawili ya kombe la FA katika kipindi cha mika mitano Old Trafford, alifurahishwa sana na ushindi wa Red Devils dhidi ya mpinzani wake wa jadi Manchester City siku ya Jumapili.
0 comments:
Post a Comment