Mchezaji wa timu
ya taifa ya England ambaye pia anakipiga katika klabu ya soka Sunderland Adam
Johnson amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na msichana mwenye
umri wa miaka 15.
Polisi katika
eneo la Durham wamesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekamatwa mapema
wiki hii kwa tuhuma za kufanya ngono na binti mwenye umri wa chini ya miaka 16,
na amebaki chini ya ulinzi.
Taarifa ndani ya
klabu yake zinasema kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kusubiri matokeo ya
uchunguzi wa polisi. Taarifa za kukamatwa kwake zilitolewa mapema kupitia
gazeti la The Sun.
Johnson akiwa na mpenzi wake mwaka 2012
Kukamatwa kwake
kunakuja muda mfupi kabla hajasafiri na timu yake ya Sunderland kwenda kukutana
na Hull kwa michezo ya Ligi kuu ya England iliyopangwa kuchezwa leo usiku.
Sunderland imesema haitaendelea kuzungumzia kukamatwa kwa mchezaji wake.
0 comments:
Post a Comment