Homa
ya Bonanza la Sports Extra Day….. au Sports Kazini Mwezi Mei… imeanza
kupamba moto, makampuni mengi yameanza maandalizi mapema kujiandaa na
bonanza hilo maarufu hapa nchini linalodhaminiwa na Clouds Media Group.
Timu ya Tanesco ambao walikuwa mabingwa wa bonanza hilo mwaka 2013
watacheza mechi ya kirafiki na timu ya Clouds Dream team siku ya
jumamosi wiki hii, Clouds pia wanajiandaa na mashindano makubwa ya NSSF
Media Cup 2015 yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo tarehe 14.
Mchezaji wa timu ya fastjet mabingwa wa mwaka jana akichuana na mchezaji wa tanesco mabingwa wa mwaka juzi.
Timu za
Fastjet ambao ni mabingwa watetezi wao wamethibitisha kushiriki katika
mikoa yote mwaka huu.
Bonanza hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya
wafanyakazi litafanyika tarehe moja mei hapa Dar Es Salaam, ikifuatiwa
na Mwanza, Arusha na Mbeya kila mwisho wa wiki katika mwezi mei 2015.
Peter Ngassa
Managing Director
0 comments:
Post a Comment