Main Menu

Monday, March 2, 2015

AZAM FC YASITISHA MKATABA NA KOCHA WAKE OMOG, MWENENDO USIORIDHISHA WATAJWA KAMA CHANZO

Baada ya kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani afrika na mwenendo usiopendeza katika ligi kuu ya vodacom,Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.

Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.


Taarifa za kufukuzwa kwake zimetolewa kupitia ukurafa wa facebook wa klabu hiyo.
 
Azam imekua na mwenendo usiovutia kwenye michezo ya hivi karibuni ya ligi kuu ya vodacom hali iliyotoa mwanya kwa timu ya yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya point nne.
 
Kwa sasa timu hiyo ipo chini ya kocha mganda George Best Nsimbe wakati masultan wakijipanga kutoa ajira kwa mwalimu mwingine ambaye hata hivyo bado haijafahamika nani ataziba nafasi hiyo.

0 comments:

Post a Comment