Timu ya Taifa ya
Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer) iliyoingia kambini mwishoni mwa
wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya
timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri mwishoni wiki ijayo.
Maandalizi ya
mchezo dhidi ya timu ya Misri yanaendelea vizuri Bamba Beach Kigamboni chini ya
kocha mkuu John Mwansasu ambaye aliingia kambini mwishoni mwa wiki na wachezaji
14.
Mchezo wa kwanza
unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini
Dar es salaam na marudio yake kufanyika baada
ya wiki moja nchini Misri.
Tanzania
ilifanikiwa kufuzu hatu ya pili baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya kwa
jumla ya mabao 12- 9, mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda kwa mabao 5-3,
na mchezo wa marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na ushindi wa
mabao 7-6.
Fainali za Mataifa
Afrika kwa Sola la Ufukweni (Beach Soccer) zinatarajiwa kufanyika mwezi April
2015 katika Visiwa vya Shelisheli.
0 comments:
Post a Comment