Wakati timu
ya yanga na azam fc zikiwa kwenye michuano ya kimataifa ligi kuu ya soka Tanzania
bara itaendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa.
Katika uwanja
wa taifa Dar es salaam wekundu wa
msimbazi Simba watawaalika maafande wa magereza Prison wakati pale katika
uwanja wa mkwakwani ndugu wa mkoa huo Coastal union na mgambo JKT wakapepetana.
Nako mkoani Shinyanga
wenyeji wa uwanja wa Kambarage Stand United na Kagera Sugar watakua katika
patashika.
Pale mbeya Timu
ya Mbeya City itawaalika maafande wa Ruvu Shooting wakitafuta ushindi baada ya
michezo minne.
0 comments:
Post a Comment