Main Menu

Wednesday, February 25, 2015

HIVI NDIVYO JULIO ALIVYOANZA KAZI COASTAL UNION

Baada ya kuipandisha ligi kuu kwa msimu ujao timu ya Mwadui fc, kocha Jamhuri Kihwelu Julio ametua timu ya Coastal kuongeza nguvu kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.

Julio atakuwepo kwenye timu hiyo hadi mwisho wa msimu kwani ikumbukwe kuwa Julio ndio aliyeisaidia timu hiyo kupanda ligi kuu.

Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri Kiwelu "Julio"kulia akisisitiza jambo mazoezini jana mara baada ya kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo kushoto ni Kocha Mkuu James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.

Kocha Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri Kiwelu Julio"akizungumza na viongozi wa Coastal Union mara baada ya kuwasili mazoezini jana ,Picha kwa Hisani ya Coastal Union

0 comments:

Post a Comment